Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uongozi wa G77 ni muhimu kuhakikisha hatua madhubuti zinapitishwa mkutano wa RIO+20:Ban

Uongozi wa G77 ni muhimu kuhakikisha hatua madhubuti zinapitishwa mkutano wa RIO+20:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mwaka huu kuna fursa ya kihistoria ya kushughulikia moja ya changamoto kubwa zinazowakabili binadamu ambayo ni kujenga dunia bora na salama. Akizungumza Jumatano katika hafla ya kukabidhi madaraka ya uwenyekiti wa G-77 Ban amesema mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu wa Rio +20 una fursa moja katika kizazi hiki ya kujenga mustakhbali wa dunia tunaoutaka.

Amesema kinachotakiwa ni kuanzisha mikakati imara ya kimataifa, kukabili changamoto zote muhimu za sera za mabadiliko ya hali ya hewa, upungufu wa maji, uhaba wa nishati, matatizo ya kimataifa ya afya, upungufu wa chakula na kuwawezesha wanawake.

Ban ameongeza kuwa suluhu ya tatizo moja lazima iwe ya matatizo yote na uongozi wa G-77 ni kitovu cha kuhakikisha hatua muhimu zinapitishwa kwenye mkutano wa Rio +20.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)