Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR akamilisha Sudan na Sudan Kusini

Mkuu wa UNHCR akamilisha Sudan na Sudan Kusini

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bwana Antonio Guterres amehitimisha ziara yake Sudan Kusini leo Jumanne na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada mkubwa wa kibinadamu katika taifa hilo jipya linalokabiliwa na changamoto nyingi.

Amesema bila msaada wa kimataifa haitowezekana kukabiliana na matatizo na Sudan Kusini itajikuta katika mtafaruku mkubwa wa janga la kibinadamu. Guterres amezuru kambi ya Doro inayohifadhi wakimbizi wa Sudan kwenye jimbo la Mabaan, na kushuhudia wengi wa wakimbizi hao 28,000 wakiwa wamechoka, wana njaa na kuwa katika hali mbaya hasa wanawake na watoto waliotembea siku kadhaa ili kupata usalama pande wa pili wa mpaka.

Mapigano ya karibuni kwenye jimbo la Kordofan na Blue Nile yamewalazimisha wakimbizi wa Sudan zaidi ya 80,000 kukimbilia majimbo ya Unity na Upper Nile na wengine 33,000 kuingia nchi jirani ya Ethiopia. Andrej Mahechic ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

Guterres pia atazuru eneo la Kassala Mashariki mwa Sudan ambako kuna wakimbizi wa muda mref duniani. Wakimbizi 70,000 wako hapo wengi ni Waeritrea walioko katika kambi 12. Kambi hizo zimekuwepo tangu miaka ya 1960.