Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 52.9 ya msaada wa fedha Haiti imetoka kwa wahisani:OSE

Asilimia 52.9 ya msaada wa fedha Haiti imetoka kwa wahisani:OSE

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mwakilishi maalumu kwa ajili ya Haiti OSE imefanya tathimini mpya ya ahadi zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi mpya baada ya tetemeko la ardhi Haiti hapo Januari 12 mwaka 2010 na kubaini kwamba katika kipindi cha mwaka 2010-2011 asilimia 52 ya fedha zilizotolewa zimetokana na wahisani wa sekta za umma.

OSE imesema asilimia 6 ya fedha hizo zimetolewa kama bajeti ya kusaidia mifumo ya serikali. Kwa mujibu wa ofisi hiyo tathimini imetokana na ahadi zilizotolewa na sekta za umma 55 kwenye mkutano wa kimataifa wa wahisani kuchangisha fedha kwa ajili ya Haiti uliofanyika Machi 31 mwaka 2010. Wahisani waliahidi dola bilioni 4.5 na hadi sasa dola bilioni 2.38 sawa na asilimia 52.9 zimeshatolewa. Hata hivyo tathimini hii haijumuishi ahadi zilizotolewa katika shughuli mbalimbali za misaada ya kibinadamu