Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha hatua ya kuondolewa kwa sheria ya hali ya dharura Fiji

Pillay akaribisha hatua ya kuondolewa kwa sheria ya hali ya dharura Fiji

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatatu amekaribisha hatua ya kuondolewa kwa sheria ya hali ya dharura kwa jamii kisiwani Fiji, kama hatua moja wapo ya kuelekea kuwa na utekelezaji kamili wa haki za binadamu nchini humo. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Pillay ameongeza kuwa sheria za hali ya tahadhari zimekuwa zikizuia haki za uhuru wa watu wa kukusanyika na kujieleleza na kuipa serikali uwezo wa kuwakamata na kuwashikilia watu. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)