Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya miaka miwili kupita tangu kutokea tetemeko la ardhi Haiti, balozi wa UM atembelea eneo hilo

Baada ya miaka miwili kupita tangu kutokea tetemeko la ardhi Haiti, balozi wa UM atembelea eneo hilo

Ikiwa imepita miaka miwili baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti, mjumbe wa ngazi wa juu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mpango wa chakula ametembelea kwa mara ya kwanza eneo hilo kwa ajili ya kutathmini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo ambalo liliharibu mfumo mzima wa taifa hilo.

Katika ziara yake hiyo ya kwanza, mwandishi wa habari raia wa Canada ambaye pia ni balozi wa hisani wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, George Stroumboulopoulos amejionea hatua zilizopigwa za kulijenga upya taifa hilo lililoko katika eneo la Caribbean.

Karibu wakazi wengi ambao nyumba zao ziliharibiwa wamerejea kwenye makazi ya kawaida, huku pia kukiimarishwa mifumo ya miundo mbinu na mahitaji mengine ya kijamii.

Umoja wa Mataifa pamoja na wahisani wake ndiyo uliochukua jukumu kubwa kukarabati maeneo yote yaliyoathiriwa na janga hilo la kimaumbile.

Balozi huyo wa hisani ametembelea pia makambi yanayotumika kuwahifadhia wale waliharibiwa nyumba zao ambako mamia ya watoto wenye umri kuanzia miezi sita wanakutikana kwa ajili ya kutambuliwa kama wapo kwenye mkondo wa kukabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo utapiamlo.