Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira ya demokrasia yanaendelea Libya:Martin

Mazingira ya demokrasia yanaendelea Libya:Martin

Watu wa Libya wanaendelea kuwa na hamasa ya kutaka kujua kuhusu haki walizozipigania kwa kuangusha utawala wa kanali Muammar Al-Gadaffi, amesema mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Ian Martin ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi kwamba serikali ya mpito ya Libya inakabiliwa na changamoto mbili kubwa za kushughulikia mara moja mahitaji ya watu na kuunda katiba ya kuaminika.

Martin amesema hali ya watu Libya inaanza kubadilika taratibu na kujikita zaidi katika masuala ambayo yalikuwa kiini cha maandamano na madai yao ya kuleta mapinduzi. Masuala hayo ni pamoja na kuimarisha utendaji wa taasisi za serikali ili zikidhi matarajio ya watu, uwajibikaji na uwazi katika masuala ya umma.

Bwana Martin amesema serikali ya mpito inajitahidi kufanya kazi katika kuimarisha hali ya sintofahamu ya usalama.