Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisi ya UM ya kuweka amani Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba usaidizi wa kifedha

Afisi ya UM ya kuweka amani Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba usaidizi wa kifedha

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuweka amani kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mazungumzo kati ya serikali na makundi ya upinzani yanazaa matunda lakini ameonya kwamba ukosefu wa fedha huenda ukahujumu jitihada za kuwapokonya silaha wapiganaji wa zamani na kudumisha usalama.

Margaret Vogt amesema kuwa upande wa serikali unatilia maanani ushauri kutoka kwa washikadau pamoja na jamii ya kimataifa. Ameongeza kwamba dola milioni 19.3 zinahitajika ili kuwabadili wapiganaji wa zamani huku bajeti ya kugharamia shughuli ya kuwapokonya silaha wapiganaji ikiwa ni dola bilioni 2.9.