Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushiriano wa mataifa ni muhimu katika kuwafikisha mahakamani wahalifu wa kivita

Ushiriano wa mataifa ni muhimu katika kuwafikisha mahakamani wahalifu wa kivita

Kuwepo suhirikiano kayika kuwasaka na kuwakamata wahalifu watoro au kutoa habari kuwahusu na jambo muhimu kwa mahakama za Umoja wa Mataifa zinahusika na uhalifu wa kivita kuhusu Yugoslavia ya Zamani na Rwanda.

Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwendesha mashtaka wa mahakama kuhusu uhalifu wa kivita nchini Rwanda ICTR Hassan Jallow amesema kwamba miaka 17 baada ya kubuniwa bado washukiwa tisa wa uhalifu wa kivita wakiwemo wanaotakiwa zaidi na mahakama ICTR hawajulikani waliko. Bwana Jallow anasema kuwatafuta na kuwakamata washukiwa hao limesalia kuwa changamoto kubwa kwa mahakama ya ICTR.