Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gbagbo awasili ICC kukabili makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu

Gbagbo awasili ICC kukabili makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo mwenye umri wa miaka 66 Jumatano amewasili kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC iliyoko The Hague Uholanzi.

Gbagbo alisamilishwa kwenye mahakama hiyo na uongozi wa serikali ya Ivory Coast tarehe 29 Novemba mwaka huu kufuatia kibali cha kukamatwa kwake kilichotolewa na mahakama ya ICC tarehe 23 Novemba.

Bwana Gbagbo anadaiwa kubeba jukumu la makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu manne ikiwemo mauaji, ubakaji na ukatili mwingine wa kimapenzi, utesaji na vitendo vingine visisvyo vya kibinadamu, makosa yanayodaiwa kutekelezwa nchini Ivory Coast kati ya Desemba 16 mwaka 2010 na Aprili 12 mwaka 2011. Mahaka inasema kuna mazingira ayanayowafanya kuamini kwamba baada ya uchaguzi majeshi ya Gbagbo yalishambulia raia Abidjan na Magharibi mwa nchi kuanzia Novemba 28 mwaka 2010 na kuendelea. Hata hivyo mahakama hiyo imesema tarehe na saa ya Gbagbo kupanda kizimbani kuanza kusikilizwa kesi yake itatajwa baadaye. Fadi El Abdallah ni msemaji wa mahakama ya ICC.

(SAUTI YA FADI EL ABDALLHA)