Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al Shabaab yapiga marufuku mashirika ya kutoa misaada nchini Somalia

Al Shabaab yapiga marufuku mashirika ya kutoa misaada nchini Somalia

Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia limepiga marufuku mashirika 16 ya kutoa misaada kati kati na kusini mwa Somalia yakiwemo ya Umoja wa Mataifa hatua ambayo huenda ikasababisha madhara kwa wale ambao tayari wameathiriwa na njaa pamoja na ukame. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu kitendo cha Al Shabaab cha kupora vifaa vya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na vya mashirika ya UM. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Wakati huo huo UNHCR inaelezea hofu iliyopo kufuatia tangazo hilo la Al Shabaab linalotolewa wakati kuna hali mbaya ya kibinadamu kati kati na kusini mwa Somalia.