Kupuuza haki za binadamu sio chaguo DPRK:Darusman

28 Novemba 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK kushirikiana na mfumo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na kuanza utekelezaji wa baaddhi ya mapendekezo ili kumaliza ukiukaji wa haki za binadamu kwa watu wa DPRK.

Marzuki Darusman amesema taifa hilo huenda ni taifa pekee leo hii ambapo halijatambua kwamba kutoshirikiana na mifumo ya haki za binadamu sio chaguo. Darusman amepewa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza hali ya haki za binadamu DPRK. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter