Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshukiwa wa utawala wa Khmer Rouge atatea vitendo vyake

Mshukiwa wa utawala wa Khmer Rouge atatea vitendo vyake

Aliyekuwa naibu katibu wa chama tawala kwenye utawala wa Khmer Rouge nchini Cambodia ameiambia mahakama inayosilikiza kesi inayomkabili kuhusu uhalifu wa kivita kuwa alijaribu kuilinda Cambodia wakati wa utawala dhalimu ulioitawala Cambodia miaka ya 70.

Nuon Chea alikuwa naibu katibu kwenye chama cha Kampuchea kwenye utawala wa kati ya mwaka 1975 na 1979 ambapo inakisiwa kuhusika na vifo vya takriban watu milioni mbili. Nuon amehukumiwa na mahakama iliyobuniwa kupitia makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Cambodia kuhusiana na mashataka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.