Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi unaposuasua Kaskazini, Kusini yaweza kuleta mabadiliko:UNCTAD

Uchumi unaposuasua Kaskazini, Kusini yaweza kuleta mabadiliko:UNCTAD

Ripoti ya mwaka 2011 ya nchi zinazoendelea kuhusu jukumu la ushirikiano wa Kusini-Kusini kwa ajili ya maendeleo inasema kwamba mabadiliko ya uchumi katika maeneo ya Kusini yanaweza kuleta fursa nzuri kwa mataifa masikini yanayoendelea, lakini mkakati wa sera unahitajika ili kuimarisha na kuendeleza ushiriaka huu unaochipuka.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD imeonya kwamba matarajio katika nchi zinazoendelea yaani LDC’s hayatapewa kipaumbele sana kama ilivyokuwa miongo iliyopita na hii inatokana na hatari ya msukosuko wa kiuchumi unaoendelea kuzikumba nchi zilizoendelea na pia mabadiliko ya kuweza kuleta usawa katika uchumi wa dunia.

Ripoti inakadiria kwamba wastani wa ukuaji wa uchumi utakwa ni asilinia 5.8 ikiwa ni asilimia 1.5 pungufu ya ilivyokuwa mwaka 2002 hadi 2008. Supachai Panitchpakdi ni Katibu Mkuu wa UNCTAD

(SAUTI YA SUPACHAI PANITCHPAKDI)