Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka washambulizi wa vikosi vya kulinda amani wachukuliwe hatua:

Baraza la Usalama lataka washambulizi wa vikosi vya kulinda amani wachukuliwe hatua:

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuanza kuchukuliwa hatua kwa wale wanaoendesha vitendo vya kuwazulu ikiwemo pamoja na kuendesha mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani. Hatua hiyo inakuja kufuatia tukio la kushambuliwa kwa vikosi vya kulinda amani vilivyoko huko Darfu ambako askari mmoja aliuwawa na wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.

Baraza hilo la usalama katika taarifa yake, limelaani vikali matukio ya namna hiyo na limesema kwamba wakati umefika kwa wahusika wa matukio kama hayo kufichuliwa hadharani .

Muungano wa vikosi vya kulinda amani vinavyoundwa kwa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID unaandamwa na matukio ya kushambuliwa mara kwa mara toka kwa vikosi vya waasi kwenye eneo hilo