Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil na WFP wazindua mradi wa kuwalisha watoto shuleni

Brazil na WFP wazindua mradi wa kuwalisha watoto shuleni

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP kwa ushirikiano na serikali ya Brazil wamezindua mradi ulio na lengo la kusaidia nchi zingine kuboresha na kusimamia programu zao za utoaji wa chakula shuleni kama njia ya kuimarisha usalama wa chakula kwenye shule.

Mkurugenzi wa WFP Josette Sheeran amesema kuwa Brazil ina ujuzi mkubwa kuhusu njia za kupambana na njaa ambao mataiafa mengine yanaweza kuiga na kuutumia. Brazil imeyapa kipau mbele masuala ya vita dhidhi ya njaa na utapiamlo suala lililoifanya kuongoza kwenye vita dhidi ya njaa.