Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo kuhusu Cyprus yapiga hatua

Mazungumzo kuhusu Cyprus yapiga hatua

Kumeripotiwa mafanikio kwenye mazungumzo ya siku mbili kati ya viongozi wa Cypriot nchini Ugiriki na Uturuki pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Mshauri maalum wa katibu mkuu kuhusu Cyprus Alexander Downer amesema kuwa Umoja wa Mataifa umefurahishwa na jinsi mazungumzo kati ya kiongozi wa Cypriot nchini Ugiriki Dimitris Christofias na kiongozi wa Cypriot nchini Uturuki Dervis Eroglu yanavyoendelea.

Mazungumzo hayo ni ya nne ambapo Ban amekutana ana kwa ana na viongozi hao katika jitihada za kukiunganisha kisiwa hicho cha Mediterranean