Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yatoa wito mpya wa kuindolea Cuba vikwazo

Mataifa yatoa wito mpya wa kuindolea Cuba vikwazo

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitaka Marekani kuiondolea Cuba vikwazo ilivyoiwekea karibu nusu karne iliyopita. Kwa mwaka wa 20 sasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likipitisha azimio la kuitaka Marekani kuondoa vikwazo vikiwemo vya kiuchumi na vya kifedha ilivyoiwekea nchi hiyo ya Caribbean.

Mwaka huu wanachama 186 kati ya wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walipiga kura ya kuunga mkono azimio hilo. Hata hivyo Marekani na Israel walipinga.