Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amlilia kiongozi wa Saudia

Ban amlilia kiongozi wa Saudia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia kifo cha mwanamfalme wa Saudia Arabia Prince Sultan bin Abdul-Aziz Al aliyefariki dunia mwishoni mwa juma kwa maradhi ya saratani. Prince Sultan ambaye alikuwa mdogo wa mfalme wa Saudia Abdullah mpaka umati unamkuta alikuwa akitumika kama waziri wa ulinzi.

Alifariki dunia mjini New York alikokwenda kwa ajili ya matibabu zaidi. Katika salamu zake, Ban amesifu harakati na mchango mkubwa alioutoa wakati wa uhai wake.