Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utoaji makazi ya muda huko Saloum Misri kukoma

Utoaji makazi ya muda huko Saloum Misri kukoma

Kuanzia jumapili makundi ya watu wanaowasili katika kambi moja iliyoko mpakani mwa nchi ya Misri, wakitokea nchini Libya sasa hawatapatiwa hadhi ya makazi kwenye eneo hilo. Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa wale waliowasili kwenye kambi hiyo Saloum kabla ya jumapili bado wataendelea kupata uangalizi.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kukoma kwa hali ya mapigano yaliyojiri kwa miezi kadhaa nchini Libya, yakisababisha mamia ya watu kuyakimbia makazi yao. UNHCR imesema kuwa iwapo makundi ya watu yataendelea kumiminika kwenye eneo hilo, basi yatawajibika kujitafutia hifadhi.