Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua shindano kwa ajili ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa

UM wazindua shindano kwa ajili ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza umezindua shindano la kimataifa kwa ajili ya kuwakumbuka waathirika wa biashara ya utumwa. Shindo hilo linatazamiwa kuchukua fursa ya pekee kwa ajili ya kuwakumbusha wana ulimwengu namna mamilioni ya waafrika walivyoteseka kutokana na biashara hiyo ya utumwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ndilo lililochukua jukumu la kuratibu shindano hilo ambalo washindani wamepewa muda wa hadi disemba 11 mwaka huu 2011 kuwasilisha kazi zao.

Kwa hivi sasa Umoja wa Mataifa upo kwenye kampeni ya kujenga kituo maalumu ambacho kitakuwa kama kumbukumbu ya biashara hiyo ya utumwa ambayo ilishuhudia waafrika wengi wakichukuliwa hadi nchi za mbali na kutumikishwa kwenye kazi ngumu.