Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Russia yataka UM kuweka zingatia la usalama wa nishati

Russia yataka UM kuweka zingatia la usalama wa nishati

Russia imeutaka Umoja wa Mataifa kuanza kuandaa mkataba wa kimataifa juu ya usalama wa nishati ili kusadia juhudi za kupatikana kwa maendeleo endelevu. Wito huo umetolewa na Waziri wake wa mashauri ya kigeni Sergey Lavrov wakati akilihutubia mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa wiki hii.

Amesema kuwa kunahitajika kuwepo kwa mashirikiano ya kimataifa ili kuweza kufanikisha shabaya ya kusukuma mbele dhima ya kimaendeleo.