Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Libya wametakiwa kuharibu silaha za kemikali:

Viongozi wa Libya wametakiwa kuharibu silaha za kemikali:

Uongozi mpya wa Libya the National Transitional Council (NTC) umetakiwa kuanza kuharibu silaha zote za kemikali nchini humo.Wito huo umetolewa na mkuu wa idara ya masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe, alipotoa taarifa kwenye Baraza la Usalama leo Jumatatu.

Bwana Pascoe amesema shirika la kupinga silaha za kemikali OPCW, linajitahidi kuweza kuthibitisha taarifa kwamba majeshi ya baraza la mpito la Libya yamegundua ghala lililo na vifaa vya kutengeneza silaha za kemikali kwenye eneo la silaha za Juffra, mili 435 Kusini mwa mji mkuu Tripoli.

Ameongeza kuwa vifaa hivyo havikuwekwa bayana siku za nyuma na ameutaka uongozi wa NTC kuchuka hatua dhidi ya vifaa hivyo, ili kuhakikisha usalama watu wote na wakiwa tayari wakaribishe wakaguzi kurejea tena nchini humo.