Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yataka Sahara Magharibi ipatiwe uhuru

Tanzania yataka Sahara Magharibi ipatiwe uhuru

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema kuwa eneo la Sahara Magharini ndiyo eneo pekee barani Afrika ambalo hadi sasa bado halijapata uhuru. Eneo hilo la Sahara Magharibi ambalo ni koloni la zamani la Hispania kwa hivi sasa linapiganiwa na Morocco inayodai kuwa kwenye himaya yake, lakini mamlaka ya ukombozi ya Polisaria inatilia ngumu mpango huo.

Rais Kikwete akizungumza kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa katika kipindi chote cha miaka 50 cha uwanachama wake kwenye Umoja huo, Tanzania imetoa mchango mkubwa kuzisaidia nchi za Afrika zinapata uhuru.

Ametaka mamlaka za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa wenyewe kuongeza msukumo ili hatimaye eneo hilo la Sahara Magharibi linafikia shabaya kujipatia uhuru wake.