Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa iko kwenye mkondo mzuri

Kamati UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa iko kwenye mkondo mzuri

Kamati ya muda iliyotwikwa jukumu la kupanga mchango ulio na lengo la kuchangisha fedha zitakazosaida nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa imetangaza kupiga hatua baada ya mkutano uliondaliwa mjini Geneva. Mpango huo wa kuchangisha fedha ni moja ya maafikiano yaliyoafikiwa ya UNFCCC na nchi kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ulioandaliwa mjini Cancun nchini Mexico.

Katibu wa UNFCCC Christiana Figueres amesema kuwa kamati hiyo kwa sasa inaelekea kukamilisha mwelekeo wa mchango huo ili uweze kuidhinishwa kwenye mkutano wa UNFCCC utakaondaliwa mjini Durban nchini Afrika Kusini.