Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM afanya majadiliano na wajumbe wa bunge la Marekani

Afisa wa UM afanya majadiliano na wajumbe wa bunge la Marekani

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC amefanya mkutano na ujumbe kutoka kwa bunge la Marekani ambapo walijadili uzalishaji wa madawa ya kulevya nchini Mexico na Colombia na usafirishaji wa madawa nchini Afghanistan, usalama wa mitandao, ulanguzi wa pesa , uharamia na usafirishaji haramu wa binadamu.

Yury Fedotov mkurugenzi wa UNODC na ujumbe huo kutoka Marekani walijadiliana masuala yanayohusu uhalifu uliopangwa , ulanguzi wa madawa ya kulevya na ugaidi kwenye mkutao uliofanyika mjini Vienna. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)