Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu hatari inayokabili makao yake

Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu hatari inayokabili makao yake

Umoja wa Mataifa hivi karibuni unatarajiwa kuendesha uchunguzi kuhusu hatari inayokabili makao yake sehemu mbali za ulimwengu kufuatia shambulizi lililotekelezwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa kwenye mji mkuu wa Nijeria Abuja ambapo watu 23 waliuawa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon aliliambia baraza la usalama ka Umoja wa Mataifa kuwa kuwa alipokea habarai kutoka kwa naibu katibu mkuu Asha–Rose Migiro aliyetembelea eneo hilo.

Jengo la Umoja wa Mataia mjini Abuja lina mashirika 26 na lina ulinzi wa hali ya juu. Shambulizi hilo limetajwa kuwa kichochoe cha kuwepo uchunguzi sio tu nchini Nigeria lakini pia sehemu zingine duniani.