Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la waongezea muda majaji wa kesi ya Yugoslavia

Baraza la usalama la waongezea muda majaji wa kesi ya Yugoslavia

 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwaongezea mipaka ya utendaji majaji wanaoendesha kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu ulitendeka wakati wa machafuko ya Yugoslavia katika miaka 1990.

 

Azma hiyo imekusudia kuipa uwezo wa kiutendaji mahakama hiyo ili kukamilisha kwa wakati zoezi la uendeshwaji wa kesi hiyo. Katika uamuzi wake wa pamoja baraza hilo sasa limewaongezea muda wa kiutendaji majaji hao hadi Disemba 31 mwaka ujao 2012 lakini pia limeanisha kipengele kingine kinachosema kuwa wanaweza kuendelea kuhuduma hadi hapo kesi hiyo itakapomalizika.