Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu asema alieleweka vibaya na maafisa nchini Bahrain

Mkuu wa haki za binadamu asema alieleweka vibaya na maafisa nchini Bahrain

Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa mazungumzo yake na waziri wa maendeleo ya kijamii nchini Bahrain yalieleweka kwa njia isiyofaa na shirika moja la habari nchini Bahrain ambalo halikuwa kwenye mkutano kati yao juma lililopita.

Shirika hilo linadai kuwa afisa huyo alitoa matamshi yanayosema kuwa habari fulani aliyopokea kuhusu Bahrain haikuwa ya ukweli. Afisa huyo wa UM kwa upande wake anasema kuwa hakutoa matamshi kama hayo na alikuwa amewaomba maafisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo kuyafanyia marekebisho. Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu anaeleza.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)