Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Orodha ya urithi wa dunia yaongezeka:UNESCO

Orodha ya urithi wa dunia yaongezeka:UNESCO

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni UNESCO leo limeyaafiki mapendekezo ya nakala ambazo wahusika wake wanaelezwa kusiasisi tangu miaka 1886.

Kwa kufanya hivyo UNESCO sasa inazitambua kazi hizo kuwa ni sehemu ya uridhi wa dunia ambazo zinapaswa kuhifadhiwa na kutuzwa.

Kuingizwa kwa kazi hizo kunaongeza idadi yake ambapo sasa inafikia jumla ya 45, kazi ambazo zinatajwa kuwa zimeorodheshwa kwenye kumbukumbu ya uridhi wa dunia. Rekodi ya kumbukumbu ya dunia inajumuisha vitu mbalimbali, ikiwemo mawe, sauti zilizorekodiwa pamoja na filamu .