Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka NAM kuunga mkono kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Ban aitaka NAM kuunga mkono kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitolea mwito jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote,kuweka nia ya pamoja ili kusaidia juhudi za kimataifa za kukabiliana na tishio linalosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa suala la tabia nchi ni eneo muhimu na ni miongoni mwa vipaumbele 3 ambavyo vinapaswa kushughulikiwa kwa ushirikiano wa baina ya Umoja wa Mataifa na jumuiya hiyo ya NAM.

Vipaumbele vingine kwa mujibu wa Ban, ni kujenga dunia salama na kupiga vita umaskini wa kupindukia.

Katika hotuba yake aliyoitoa mjini Bali, Indonesia ambako kunafanyika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuasisiwa kwa jumuiya hiyo, Ban kupitia mwakilishi wake amesema kuwa suala la mabadiliko ya tabia nchi haliwezi kupatiwa ufumbuzi bila kwanza kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja.