Skip to main content

Japan yachukua tahadhari kupunguza hatari ya kuvuja kwa vinu

Japan yachukua tahadhari kupunguza hatari ya kuvuja kwa vinu

Serikali ya Japan imechukua kila tahadhari ili kukabiliana na hatari ya kutokea kwa maradhi ya saratani ambayo yanaweza kusababishwa na kuvuja kwa mionzi hatari kutoka kwenye vinu vya kinyuklia vilivyoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi na gharika ya tsunami.

Kwa sasa Japan imehamisha kila mtu kutoka eneo hilo ambapo viwango vya mionzi ni vya juu. Msemaji wa shirika la afya dunia Gregory Hartl anasema kuwa athari za kuvuja kwa mionzi hiyo bado hazijafahamika.