Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga kwa wakosaji wa haki za binadamu lazima iondoshwe Haiti:Mtaalamu wa UM

Kinga kwa wakosaji wa haki za binadamu lazima iondoshwe Haiti:Mtaalamu wa UM

Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadmu Michel Forts, amewataka wagombea urais nchini Haiti kutilia msukumu kuondosha mfumo wa kukwepa kuwajibisha pindi wapokwenda kinyume na haki za binadamu.

Amesema wakati taifa hilo linajiandaa na uchaguzi mkuu, ni vyema kuzingatia kuwa inajiweka kando na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu.

Ametaka kufanyika kwa mageuzi ya kubadilisha mifumo na taratibu ambayo iliwajengea uwigo baadhi ya viongozi kutofikishwa kwenye mikono ya sheria wakati wanapokiuka haki za binadamu.

 

Mtaalamu huyo ameeleza kuwa kikwazo kimojawapo kinachorudisha nyuma ustawi wa haki za binadamu ni kutokana na kinga iliyopo kwa baadhi ya watendaji ambao inawafanya waendelee kupuzia haki za binadamu.