Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya uchaguzi Afghanistan lazima iruhusiwe kutimiza jukumu lake:UM

Tume ya uchaguzi Afghanistan lazima iruhusiwe kutimiza jukumu lake:UM

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura leo ameipongeza tume ya uchaguzi nchini Afghanistan kwa kuendesha uchaguzi wa bunge wa hivi karibuni kukiwa na hofu ya usalama changamoto za kiufundi.

De Mistura amesisitiza kuwa tume hiyo lazima ipewe fursa ya kukamilisha majukumu yake. Zaidi ya wapiga kura milioni 4 walishiriki uchaguzi wa Jumamosi iliyopita wa bunge la nchi hiyo Wolesi Jirga ambao uliandaliwa na tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo IEC.

Amesema tume hiyo hivi sasa iko katika hali ngumu na muhimu ya kutekeleza majukumu yake ya kukamilisha uchaguzi wa bunge, amesema licha ya matatizo wamezingatia ratiba ya uchaguzi kupiga hatua kubwa katika kuendesha uchaguzi.