Skip to main content

Mkuu wa UNESCO amelaani mauaji ya mwandishi habari wa Kimexico:

Mkuu wa UNESCO amelaani mauaji ya mwandishi habari wa Kimexico:

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ambalo pia linajukumu la kulinda uhuru wa vyombo vya habari leo amelaani mauaji ya mwandishi habari wa Mexico.

Mwandishi huyo Hugo Alfredo Olivera Cartas mwenye umri wa miaka 27 alikutwa amekufa kwenye gari lake Julai 6 mwaka huu karibu na mji wa Apatzingan kwenye jimbo la Magharibi la Michoacan. Olivera alikuwa anaripoti habari zinazohusiana na uhalifu. Kifo chake kinafanya jumla ya waandishi habari waliouawa mwaka nchini humo kufikia wanane.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la waandishi habari wasio na mipaka RSF bwana Olivera alipokea simu ikimtaka aende mahali palipotokea ajali. Maiti yake ilikutwa saa kadhaa baadaye ikiwa na majeraha matatu ya risasi kichwani na ofisi yake ilivamia baadaye.

Mkuu wa UNESCO Irina Bokova ameitaka serikali ya Mexico kuwatafUta na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahisika wa mauaji hayo.