Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rekodi mpya ya dunia imewekwa na azimio la kimataifa la haki za binadamu

Rekodi mpya ya dunia imewekwa na azimio la kimataifa la haki za binadamu

Azimio la kimataifa la haki za binadamu limevunja rekodi ya dunia kwa kuwa ndio nyaraka iliyotafsiriwa katika lugha nyingi duniani.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imepokea cheti kutoka kitengo cha kimataifa cha rekodi, Guiness Book of records kikieleza kwamba azimio hilo la haki za binadamu limetafsiriwa katika lugha 370 kuanzia Abkhaz hadi Kizulu.

Muongo mmoja uliopita azimio hilo lilipata cheti cha kuwa ndio nyaraka iliyotafiriwa sana lakini ilikuwa ni kwa lugha 298, na tangu hapo ofisi ya haki za binadamu imekuwa ikipokea tafsiri kutoka lugha nyingine mbalimbali.