Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kusaidia watoto walioathirika na tetemeko la ardhi Uchina

UNICEF kusaidia watoto walioathirika na tetemeko la ardhi Uchina

Nchini Uchina wakati jopo la waokozi likiendelea kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi kwenye mji wa Jiegu, imebainika kuwa majira ya baridi yanahatarisha maisha ya maelfu ya watoto.

Mwishoni mwa wiki watu wengi walilazimika kulala katika maeneo ya wazi huku kukiwa na nyuzi joto sufuri. Hivi sasa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linachukua hatua za kusaidia kufuatia maombi ya wizara za afya na elimu na kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa.

UNICEF inaratibu misaada yakle hasa kwa kuangalia maslahi ya watoto na katika siku chache zijazo itapeleka jozi 5000 za nguo za baridi za watoto, mahema 150, na mablanketi 2000. Kufikia leo idadi ya waliokufa inakaribia 2000, huku wengine 256 hawajulikani waliko na zaidi ya elfu 12 wamejeruhiwa. Watu zaidi ya elfu sita wameokolewa , watu laki moja wamepoteza nyumba zao na asilimia 85 ya majengo yote yamebomolewa.