Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu kuchunguza ukiukaji haki Israel na Palestina

Baraza la haki za binadamu kuchunguza ukiukaji haki Israel na Palestina

Baraza la haki za binadamu leo limepiga kura ya kuunda kamati itakayofuatilia uchunguzi wa Israel na Palestina katika madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.

Baraza hilo limepitisha azimio la kuunda kamati itakayojumuisha wataalamu wa kujitegemea wa masuala ya kimataifa na sheria za haki za binadamu ili kuangalia na kutathmini yote yatakayofanywa kijamii na kisheria na pande zote , Israel na Palestina.

Marekani, Italy na Uholanzi wamepiga kura ya kupinga azio hilo lililopendekezwa na jumuiya ya Kiarabu na nchi za Kiislam. Navi Pillay ni kamishina mkuu wa haki za binadamu.