Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Craig David ateuliwa kuwa Balozi Mwema wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB)

Craig David ateuliwa kuwa Balozi Mwema wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB)

Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya pop Craig David ameteuliwa kuwa balozi mwema wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB).

Mwanamuziki Craig David amekuwa ni mmoja wa mabalozi wema wapya wa kuusaidia Umoja wa Mataifa kuchagiza masuala mbalimbali.

Bwana David atafanya kazi na vuguvugu la kimataifa la kupambana na Kifua Kikuu lijulikanalo kama "Stop TB partnership". Tangazo la kuteuliwa kwake, limetolewa leo hapa mjini New York na Shirika la Afya Duniani WHO katika hafla ya kuazimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani ambayo husherehekewa kila mwaka tarehe 24 Machi. WHO inakadiria kuwa Kifua Kikuu kinaua watu milioni 1.8 kila mwaka. Kila mwaka kuna visa miloni tisa vya kifua kikuu na watu bilioni mbili ambo ni theluthi ya watu wote duniani wameathirika na virusi vinavyosababisha Kifua Kikuu.

Craig David anasema kwake ni muhimu kutembelea nchi ambazo zimeathirika na Kifua Kikuu kama balozi mwema na kuhakikisha kwamba ugonjwa huo haupuuzwi. "Bila shaka kwenye matamasha yangu nitaonyesha picha za athari ya ugonjwa huo na nitauzungumzia amesema David. " Ameongeza kuwa kwake itakuwa muhimu zaidi kwani atawafikia mamilioni ya watu katika hali kama hiyo, akizungumzia akijua kuwa katika habari watu watapenda kujua kuwa mwanamuziki anajukua jukumu lingine pia mbali ya kuimba. Amesema Kifua Kikuu hakipati kani tuu katika nchi zinazoendelea bali pia hata katika miji kama New York na London.