Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali katika Somalia

Hali katika Somalia

Makala ya wiki hii leo inazungumzia matatizo na vita vinavyoendelea kuikumba Somalia kwa takriban miongo miwili sasa. Kwa mujibu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanyoendesha shughuli zake nchini Somalia mwezi wa Januari mwaka huu umeghubikwa na giza nene la vita vikali.

Watu zaidi ya 258 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejuruhiwa huku maelfu wakizikimbia nyumba zao kuacha bila ya makazi. Somalia imekuwa bila serikali maalumu kwa karibu miongo miwili sasa. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimewaacha watu milioni 1.4 kuwa wakimbizi wa ndani.

Utasikia uchambuzi wa mwandishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali hiyo, pia mkaazi wa Mogadishu anavyoathirika na machafuko hayo yasokwisha. Na je upande wa serikali unasemaje? Ungana nami Flora Nducha.