Wito wa utulivu watolewa, ghasia zikiongezeka Ivory Coast
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast umeshuhudia ghasia hivi karibuni kwenye miji ya Katiola na Divo, na umetoa wito wa kuwepo na hali ya utulivu wakati shughuli ya uandikishaji wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu ujao ikifanyika.
Uandikishaji huo wa awali unafanyika hivi sasa katika maandalizi ya kutoa orodha ya mwisho ya wapiga kura, hatua ambayo ni muhimu sana katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu.
Mpango huo wa kulinda amani ujulikanao kama UNOCI umezichagiza pande zote kushirikiana kutatua masuala nyeti huku wakiheshimu sera zao.