Skip to main content

OHCHR imepeleka timu ya wataalamu wa haki za binadamu Gabon kufuatilia uchaguzi wa uraisi

OHCHR imepeleka timu ya wataalamu wa haki za binadamu Gabon kufuatilia uchaguzi wa uraisi

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR) imetuma wataalamu wanne nchini Gabon, kuchunguza hali ya haki za binadamu, kwa ujumla, wakati uchaguzi wa uraisi unapofanyika katika taifa hili la Afrika Magharibi.

Timu ya UM inatazamiwa kuwepo Gabon kwa muda wa wiki mbili, na itasaidiwa na wataalamu wenyeji, kwa ushirikiano, vile vile, na Serikali ya Gabon kwa makusudio ya kuhakikisha haki za binadamu zinahishimiwa na watu wote wakati wa uchaguzi. Miongoni mwa mambo ambayo yatachunguzwa na wataalamu wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa haki za umma, kushiriki kwenye shughuli za jamii bila vizingiti, uhuru wa kutoa mawazo na kujieleza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kutokamatwa kihorera au kuwekwa kizuizini bila ya sheria. Vile vile wataalamu hawa wa UM watawashauri na kuwahisisha makundi mbalimbali yanayotayarisha uchaguzi juu ya masuala yanayohusu haki za binadamu.