Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inasema wahamiaji 86,000 wamen'golewa makazi Mogadishu

UNHCR inasema wahamiaji 86,000 wamen'golewa makazi Mogadishu

UNHCR imeripoti kwamba kuanzia tarehe 08 Machi mwaka huu, hadi hivi sasa, jumla ya raia waliokosa makazi katika mji wa Mogadishu, Usomali kutokana na mapigano imefikia watu 86,000.

Taarifa hiyo ilibainisha watu 30,000, kati ya idadi hiyo, waling'olewa makazi ndani ya mji wa Mogadishu, na raia 25,000 walihamia eneo la Afgooye, wakati idadi iliosalia ililazimika kuhama mastakimu kutoka sehemu nyengine za nchi. Juu ya hayo, watu 3,700 waliong'olewa makazi kati ya raia 86,000 waliarifu UNHCR kuwa wanataka kuondoka Usomali na kuelekea mataifa ya nje - 600 yao wamesema wanataka wapelekwe Ethiopia, 2,000 watakwenda Kenya na wahamiaji 1,100 wengine wanajiandaa kuelekea Yemen na Saudi Arabia.