Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukio la mripuko Tanzania bado linaathiri kihali maelfu ya raia

Tukio la mripuko Tanzania bado linaathiri kihali maelfu ya raia

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) imeripoti maelfu ya raia wa Tanzania waliong’olewa makazi, wiki tatu nyuma, kwenye eneo la Dar es Salaam liliopo karibu na kambi ya kijeshi, bado wanaendelea kuishi kwenye mazingira magumu na wanahitajia kufadhiliwa misaada ya dharura, ya kihali, kwa muda mrafu ujao, kumudu maisha.

IFRC imeanzisha kampeni maalumu sasa hivi ya kuchangisha msaada wa dharura wa dola 450,000, kuusaidia kihali umma huo. Julius Kejo, meneja anayehusika na huduma za kudhibiti maafa, kutoka tawi la Msalaba Mwekundu Tanzania, amenakiliwa akisema "watu 20,000 waliopoteza makazi kwa sasa  ... wanahitajia mahema na kadhia nyengine za kihali, huduma ambazo zitawapatia waathirika hawa angalau hadhi wastani ya kiutu kumudu maisha."