Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC imekanusha tetesi za BBC juu ya uhusiano wa CNDP na MONUC

MONUC imekanusha tetesi za BBC juu ya uhusiano wa CNDP na MONUC

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limekanusha kihakika tetesi za ripoti ya shirika la habari la Uingereza la BBC zinazodai John Bosco Ntaganda, mtuhumiwa wa jinai ya vita na kiongozi wa kundi la waasi la CNDP kwenye eneo la kaskazini-mashariki ya JKK, alishiriki kwenye operesheni za vikosi vya UM nchini mwao.

Taarifa ya MONUC ilikumbusha Ntaganda, anayejulikana kwa jina la utani kama "Mkomeshaji Matatizo"/Terminator, ni mtuhumiwa mtoro anayetafutwa na mahakama ya UM juu ya uhalifu wa vita, kwa makosa ya kuteka nyara watoto wadogo na kuwalazimisha kushiriki kwenye mapigano.