Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Hapa na pale

Kabla ya kuelekea New York mnamo Ijumatatu ya leo KM Ban Ki-moon asubuhi alihutubia Kikao cha Pili cha Taasisi ya Kimataifa kuhusu Ushirikiano wa Kitamaduni katika mji wa Istanbul, Uturuki. Taasisi hii, ilioanzishwa kuziba pengo liliojiri la kutofahamiana kati ya tamaduni za mataifa ya magharibi na ulimwengu wa KiIslam, inahudumiwa shirika Serikali za Uturuki na Uspeni, zikisaidiwa na UM. Alisema KM kwenye hotuba yake kwamba Taasisi ya Ushirikiano wa Kitamaduni ina matumaini ya kutia moyo yatakayowapatia walimwengu "fursa ya kushirikiana katika kuachana na sera za mgawanyiko zinazopaliliwa na hitilafu za kikale, na badala yake kuimarisha fungamano za kiutu, za kimaumbile, miongoni mwa jamii moja ya wanadamu."

Tunzo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa 2009, inayotolewa na Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kila mwaka safari hii ametunukiwa, baada ya kufariki, mwandishi habari wa Sri Lanka, Lasantha Wickrematunge ambaye aliuawa tarehe 08 Januari mwaka huu. Timu ya waandishi habari wa kulipwa 14, kutoka sehemu mbalimbali za dunia, walimteua Wickrematunge kupokea Tunzo ya UNESCO kwa sababu ya msimamo wake kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, msimamo ambao tume ilisisitiza, unaendelea kuwahamasisha waandishi habari katika sehemu ya kadha wa kadha za dunia. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Koichiro Matsuura atawasilisha Tunzo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa 2009 kwenye taadhima maalumu itakayofanyika tarehe 03 Mei, siku ambayo huadhimishwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.