Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simu za mkono njia muhimu ya mawasiliano kwa mataifa maskini

Simu za mkono njia muhimu ya mawasiliano kwa mataifa maskini

Sita kati ya kila watu kumi kote duniani wanasimu ya mkono ikiwa ni ishara kwamba simu hizo ndizo teknolojia ya mawasiliano iliyochaguliwa hasa katika mataifa maskini, hiyo ni kufuatana na ripoti mpya ya UM.

Idara ya kimataifa ya mawasiliano ITU ya UM, imeeleza kwamba kufikia mwishoni mwa mwaka jana kulikua na simu bilioni 4.1 zilizokodishwa kulingana na bilioni moja 2002. Na inakisiwa kwamba asili mia 23 ya wakazi wote duniani wanatumia mtandao wa tovuti ukilinganisaha na asili mia 11 mwaka 2002. Kufuatana na ripoti hiyo mataifa ya ulaya kaskazini yakiongozwa na Sweden yako mbele kabisa na ufundi wa mawasiliano ya simu ya mkono na tovuti isipokua Korea ya Kusini iliyochukua na fasi ya pili mbele ya Denmark. Takwimu hiyo ya ITU ililinganisha maendeleo katika nchi hizi katika kipindi cha miaka mitano kwa kupima idadi ya komputa katika kila nyumba, idadi ya watumizi wa tovuti na idadi ya simu za mikono. Ripoti hiyo hata hivyo, imegundua kwamba mwanya mkubwa katika teknolojia ya kompyuta umebaki pale pale, kati ya walokua nao na wasio nayo licha ya manedeleo makubwa yaliyopatikana katika nchi zinazoendelea.