Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura wahitajika Somalia

Msaada wa dharura wahitajika Somalia

Idara ya kuratibu huduma za dharura za UM, OCHA imeonya kwamba bila ya kuongezwa haraka msaada kukabiliana na janga kubwa la utapia mlo na magonjwa huko Somalia, basi hali hiyo itazidi kuzorota.

Katika onyo lililotolewa, idara hiyo inasisitiza haja ya msaada wa dharua wa lishe bora pamoja na maji masafi na huduma za usafi katika majimbo mawili ya kaskazini na kati ya Somalia. Zaidi ya dola milioni 20 zinahitajika kwa ajili ya mahitaji ya chakula kwa miezo minne ijayo.