Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanyarwanda wa JKK waiomba UM iwarejeshe makwao

Wanyarwanda wa JKK waiomba UM iwarejeshe makwao

Idadi kubwa ya raia wa Rwanda wameonekana wakiibuka kutokea mafichoni kwenye maeneo ya mbali katika eneo la mashariki la JKK wakiiomba UNHCR iwarejeshe makwao, UM umeamua kuongeza idadi ya magari yatakayohitajika kuhamishia umma huo, na kumefunguliwa vituo ziada katika Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, ili kuwapatia makazi ya muda watu 500 kabla ya kuhamishiwa makwao.