UNODC inahimiza utawala bora Afrika Mashariki

6 Februari 2009

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imeripoti kuibuka mkondo mkali wa uhalifu wa mpangilio, ulionekana kushtadi kwenye mataifa yaliopo ukanda wa Afrika Mashariki. Mkondo huu unahitajia kudhibitiwa mapema kabla haujasambaa zaidi kieneo na baadaye kuhatarisha usalama, inasema UNODC.

Ofisi ya UM Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imethibitisha Mataifa ya Afrika Mashariki yanakabiliwa na mfululizo wa vitendo kadha wa kadha vya uhalifu, vinavyojiandaa kulivamia eneo hilo, kutokana na suala la kupamba kwa mizozo kieneo. Vile vile masuala yanayohusu utawala dhaifu na utekelezaji wa sheria ulioregarega, ni hali ambayo pia huwapa fursa wahalifu wa kimataifa, na kizalendo, kuamua kuendeleza vitendo vyao katika nchi za Afrika Mashariki.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud