Skip to main content

Mjumbe wa KM Usomali alaani vikali mauaji ya kihorera ya watu mashuhuri nchini

Mjumbe wa KM Usomali alaani vikali mauaji ya kihorera ya watu mashuhuri nchini

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould Abdallah kwenye taarifa iliotolewa leo Ijumaa, amelaani mauaji ya karibuni ya watu mashuhuri watatu katika Usomali, na kusisitiza kwamba vitendo vya “uhalifu” na jinai isiyokhofu kuadhibiwa wala kuumia, ni lazima vikomeshwe haraka nchini humo.